Monday, December 3, 2012

Rais Kikwete aahidi Msaada wa Bajaji kwa mlemavu Mwendo Saidi Lindi Lindi vijijini


Rais Jakaya Kikwete akizungumza na  mlemavu Mwendo Said wa Lindi vijijini wakati alipokutana naye katika ziara yake aliyoifanya jana mkoani  Lindi na kuahidi Msaada wa Bajaji kwa ajili ya kurahisisha usafiri wake na kumsaidia katika shughuli zake za kila siku.
PICHA NA FREDDY MARO WA IKULU


Rais Kikwte azindua Jengo la Mahakama ya Mwanzo Rondo,Lindi vijijini

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Jaji  Kiongozi Fakhi
Jundu(kushoto),Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Bernard Membe(watatu kulia) na mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick
Mwananzila wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Mahakama ya
Mwanzo lilijengwa kwa nguvu za wananchi na wafadhili katika kata ya
Rondo,jimbo la Mtama,Lindi vijijini jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Jaji Kiongozi Fakhi Jundu
wakikagua jengo jipya la mahakama ya Mwanzo lililojengwa kwa nguvu ya
wananchi na wafadhili mbalimbali katika kata ya Rondo, jimbo la
Mtama,Lindi vijijini jana(picha na Freddy Maro)

HAFLA YA MIAKA 20 YA CLUB BILICANAS NA MIAKA 13 YA CLOUDS FM YAFANYIKA

Keki iliyoandaliwa kwa ajili ya hafla hiyo
Dk. Lilian Mtei akikata katika hafla ya klabu Bilicanas kutimiza miaka 20 ya utendaji wake wa kazi katika tasnia ya Burudani iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
………………………………………………….
Na Andrew Chale
 
WADAU  mbalimbali  wa burudani  usiku  wa kuamkia jana walifurahia kwa pamoja  na kula keki ya miaka 20 ya klabu ya Kimataifa ya Bilicanas na miaka 13, ya Clouds Fm,  iliyoambatana na shamrashamra mbalimbali ndani  na nje ya  ukumbi huo.
 
Sherehe hizo ziliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bilicanas Group, Dk. Lilian Mtei  ambapo aliwashukuru wadau hao kwa kuwa bega kwa bega na klabu hiyo, tangu 1992. “Tunawashukuru sana kwa kuwa nanyi mara zote inatia faraja kwetu na tutaendelea kutoa huduma bora siku zote|” alisema Mbowe.
 
Mtei pia aliwashukuru wafanyakazi mbalimbali waliofanikisha ukumbi huo kufikia hapo na kutoa heshima ya kipekee kwa wafanyakazi  waliokuwapo  tokea inaanza hadi ilipofikia miaka 20 na hatimaye  kukata keki hiyo.
 
“Uwepo wa miaka 20, tuna kila sababu ya kuwapongeza wafanyakazi  tuliokuwa nao toka mwanzo hadi leo, na kwa heshima ya pekee  Mama Victor na Mrs Mitemo  ndiyo watakao kata keki hii” alisema Mtei.
 
Keki hiyo ilikatwa na wafanyakazi   hao  Monica  Victor   na Pili Mitemo  ambaye alimwakilisha mumewe aliyekuwa Meneja wa kwanza wa klabu hiyo, ambaye kwa sasa ni marehemu.
 
Aidha, kwa upande  Clouds FM, iliwakilishwa na Wasiwasi Mwabulambo ambaye alipongeza klabu Bilicanas kwa kuwa mstari wa mbele katika kuinua sanaa nchini hasa kwa kuwasaidia wasaidia wasanii kufikia malengo yao.
 
Kwa upande wake  Ibrahim Tuwa ‘Dj Ibra’ aliyekuwa akisherehesha  shughuli hiyo, aliwaomba wadau kuendelea kuwaunga mkono na wataendelea na huduma bora zaidi ha hapo. Dj Ibra alijiunga na Bilicanas tokea 2002,ambapo mpaka sasa ana miaka 10 kwenye klabu hiyo  iliyowahi kuwa na madj maarufu waliopita  hapo ambao wengi wao wapo kwenye vituo vya televisheni na redio.

No comments:

Post a Comment