Sunday, November 18, 2012

MAKUBWA YATOKEA

Stori: Shakoor Jongo
SIKU chache baada ya mazishi ya aliyekuwa mwimbaji wa Taarab wa Kundi la Tanzania One Theatre ‘TOT’, Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’ (pichani)aliyefariki usiku wa Novemba 12, mwaka huu wakati akijifungua kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, mazito yameibuka.
Mume wa marehemu Mariam, Haji Kijungu akiwa makabirini
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichohudhuria mazishi hayo yaliyofanyika Novemba 14, mwaka huu katika makaburi ya Ndugumbi, Magomeni Makuti jijini Dar, baada ya mazishi watu walionekana…
Stori: Shakoor Jongo
SIKU chache baada ya mazishi ya aliyekuwa mwimbaji wa Taarab wa Kundi la Tanzania One Theatre ‘TOT’, Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’ (pichani)aliyefariki usiku wa Novemba 12, mwaka huu wakati akijifungua kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, mazito yameibuka.
Mume wa marehemu Mariam, Haji Kijungu akiwa makabirini
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichohudhuria mazishi hayo yaliyofanyika Novemba 14, mwaka huu katika makaburi ya Ndugumbi, Magomeni Makuti jijini Dar, baada ya mazishi watu walionekana kujikusanya makundi-makundi na kuanza kujadili yaliyotokea.
Katika majadiliano hayo yaliyokuwa yakiendelea makaburini, watu waliokuwa jirani na marehemu, walitupa lawama zao kwa mfanyabiashara mmoja maarufu Bongo (jina linahifadhiwa) wakimtuhumu kuwa alimpa ujauzito marehemu huku akifahamu fika kuwa alikuwa ni mke wa mtu.
Wafiwa wakilia kwa uchungu
“Kila mtu ana aibu yake hapa duniani lakini hii ya huyu mfanyabiashara ya kutembea na mke wa mtu mpaka kumpa ujauzito uliosababisha mauti yake ni zaidi ya aibu, sijui atauficha wapi uso wake,” alisikika msichana mmoja akiwaambia wenzake.
Chanzo chetu kilieleza kuwa baadhi ya watu waliokuwa makaburini hapo, walienda mbali zaidi na kudai kuwa kifo cha Mariam kilisababishwa na msongo wa mawazo alioupata kwani inadaiwa baada ya mfanyabiashara huyo kutambua kosa lake, aliukana ujauzito huo na  kumtaka Mariam arudi kwa mumewe.
“Unajua Mariam huku mwishoni alipata ‘stress’ kubwa sana, yule mfanyabiashara alimpa makavu na kumtaka arudi kwa mumewe, akakataa kuendelea kumhudumia marehemu na mzigo wake, nadhani hii ni miongoni mwa sababu zilizoukatisha uhai wake,” alisikika dada mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Khadija, mkazi wa Magomeni Mapipa.
ALICHOKISEMA MUME WA MAREHEMU
Mume wa marehemu, Haji Kijungu aliyefunga naye ndoa miaka mitano iliyopita, naye alizungumzia pigo alilolipata huku akionesha kuumizwa sana na kifo cha mkewe ambaye tayari alizaa naye mtoto mmoja aitwaye Tariq.
“Naumia sana na kifo cha mke wangu, angenisikiliza haya yote yasingetokea. Nilikuwa namsihi kila siku arudi nyumbani tuje tumlee mtoto wetu (Tariq) lakini hakunisikia kwani alishazama kwenye penzi la… (anamtaja mfanyabiashara huyo). Yote namwachia Mungu kwani yeye ndiyo anayejua kila kitu kilichopo hapa duniani.
“Natamka kuwa nimemsamehe mke wangu kwa yote aliyonitendea enzi za uhai wake, tazama ameniachia Tariq nimlee peke yangu,” alisema mume huyo wa marehemu kwa sauti ya majonzi iliyofuatiwa na kilio cha maombolezo.
Mariam ameacha watoto wawili, mmoja wa kiume (Tariq) aliyezaa na mumewe wa ndoa na mwingine mchanga wa kike, aliyepoteza maisha wakati akimleta duniani.

Tamasha la Makuya‏

Posted by GLOBAL on November 17, 2012 at 4:11pm 2 Comments
Wasanii wa moja kati ya Vikundi vinavyoshiriki Tamasha la ngoma za Asili za makabila ya watu wa Mkoa wa Mtwara  la MaKuYa wakifanya onyesho la Ngoma katika Uwanja wa Nangwanda Mjini Mtwara. Tamasha hilo la Siku mbili  limevuta hisia za wakazi wengi wa mji wa Mtwara.…

No comments:

Post a Comment