TEMEKE PAMOJA CLASSIC WEAR YAKUTANISHA WATOTO WA TEMEKE
Waendeshaji wa blog ya TemekePamoja (KC mwenye flana ya kijani na
Ramaraldo flana nyeusi uwanja wa ndege wa Mwalimu nyerere D`Salaam)
Huyu ni rafiki yangu toka kitambo sana kabla yeye ajawa KC Mwenye Kijani
na mimi sijawa Raldo .Kwapamoja tumekaa chini na kujipanga katika mikakati
ya life ya bongo na nje ya bongo na kwa upande wa bongo tumeanza na duka la
nguo kuangalia upepo unaendaje.Watu wetu tegemeeni vitu vingi vitakuja
ndani ya temekepamoja si tu biashara ya nguo kuna biashara nyingi
zitakazoletwa na temekepamoja.Kwanini tumeamua kuwa temekepamoja na si
Darstockhom?Tumefi... more »
HUYU NDO MTOTO WA MIAKA MITATU ULIYEKUWA UKIMSIKIA KWENYE HEKAHEKA TOKEA JUZI NDO HUYU HAPA KATIKA PICHA JINSI ALIVYO FANYIWA UKATILI WA AJABU NA MAMA YAKE MDOGO

*Mtoto ANETH anavyoonekana jinsi alivyounguzwa na mama yake mdogo*
*HIVI NDIVYO ALIVYOUNGUZWA MTOTO ANETH NA MAMA YAKE MDOGO*****
*HUYU NDIYO MAMA MDOGO WA ANETH AMEJULIKANA KWA JINA LA BAHATI LUKANGARA
NDIYO ALIYEMUUNGUZA MTOTO ANETH*
*HAPA MAJIRANI WAKIJARIBU KUMUULIZA SABABU ZA KUMUUNGUZA HUYO MALAIKA WA
MUNGU NINI SABABU YAKE MPAKA AKACHUKUA HATUA YA KUMUUNGUZA LAKINI KWA
KIBURI CHA HUYO MAMA ALIKAA KIMYA KABISA BILA YA KUJIBU CHOCHOTE***
*MWENYEKITI WA MTAA HUO HABIBA MWAKITALU AMEMBEBA MTOTO ANETH TAYARI KWA
KUMPELEKA HOSPITALI HUKU NYUMA AKIFUATIWA NA MWESHIMIW... more »
Chereko- Baba kapata Mama!
Baada ya shughuli ya mahari kwenye shughuli ya Macarios ilibidi ndugu
waserebuke pichani kutoka kushoto dada Mwenda na Dada Appia wakicheza kwa
furaha
Pete ya uchumba
Bw. Macarios Banzi akimvisha pete ya uchumba Bi Martina Jeremias katika
hafla fupi na ya kufana iliyofanyika nyumbani kwa Bi Martina - Gongo la
Mboto mwisho wa lami tarehe 11/11/2012.HONGERA SANA DOGO!
KERO YA KARIAKOO MCHANA

Nipo Kariako mda huu jua ni kali msongamano wa magari, na hayatembei
hatari tupu barabara zote zimefunga
Hali kama hivi
Na kila mtu ana haraka njia hazipitiki
Maeneo ya kituo cha polisi cha kamata kuefunga
Foleni inaendelea
Hapa ndio niliposimamia wadau unabidi ujipange kwa sasa hivi ukiwa unakuja
mitaa ya kariakoo mchana.
SOKO KUU LA TEMEKE LEO

Nazi kama zinavyoonekana bei ya leo kuanzia 250.
Usafi katika soko ukiendelea
Ila wanatimua sana vumbi inatakiwa muwe mnafagia usiku
Hapa ilibidi nisimame kidogo nipate kitu cha samaki wakavu ili mchana uwe
mzuri
Matikiti Maji 400 na kuendelea
Matunda kibao pensheni kilo 500
Nanasi bei poa kuanzia 300
huu upande wa matunda
MATAYARISHO YA FILAMU YA TEARS ON MY BIRTHDAY-MBEYU MAXWELL

Muhusika mkuu wa filamu anaitwa Bonita akiwa na Director ambaye ni
mjerumani jina lake ni Andrea Lauterbach
Picha ya pili ni sehemu ya mchezo huo, ambapo muhusika mkuu Bonita au jina
la filamu Aminata akiwa na mpenzi wake Benjamin Hoesch (jina la filamu
Robert)
Moja ya filamu ambayo tayari imeshaisha ya Mbeyu Maxwell
Mbeyu Maxwell mwenye flana ya njano ambaye anasimamia mzigo wote wa filamu
hizo.
HEPI BETHDEI MH. TEMBA

Leo ni siku ya kuzaliwa ya mtoto wa TMK Aman James Temba blog ya
Temekepamoja inakutakia maisha mema na marefu
Mh. John Malecela 1977

Wakati huo Mzee John Malecela alikwa Waziri wa Kilimo. Na hapa anapokea
cheki ya shilingi 1,000/= kutoka kwa Mkuu Gereza la Lilungu Mkoani Mtwara
ikiwa kama mchango wa gereza kwa CCM!(Picha kwa hizani ya Gazeti la
DailNews 8/11/2012)
Nani atamsaidia huyu?

Anataka kufikisha kwa mlaji lakini pia anakwepa gharama kubwa ya
usafirishaji kwa kutumia vyombo vya moto ndiyo maana anasafirsha kwa
kutumia baiskeli. Angalia jinsi tenga moja la nyanya linavyotaka kudondoka!
Wahandisi mko wapi kumsaidia huyu jamaa? (Picha kwa hisani ya gazeti la
Dailynews)
Watafiti wa Kilimo hakuna kulala
Watafiti wa sekta ya kilimo kwa kupitia programu na miradi mbalimbali
wanajitahidi kuhakikisha kuwa nchi inazalisha chakula kingi na chenye ubora
wa hali ya juu na pia kuwaongezea kipato wakulima na kuboresha maisha
yao.Mradi wa SIMLESA unaotekelezwa katika wilaya za Mbulu, Karatu, Mvomero,
Kilosa na Gairo ni moja kati ya miradi inayolenga huko. Pichani Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo Bi. Ruth Kamala akitoa hotuba ya
ufunguzi wa mkutano huo.Picha na Livingstone Mwedipando wa ARI-Selian,
Arusha)
Arusha wanavyotunza mazingira
Hii ni moja ya barabara za jiji la Arusha inayokwenda kwenye kitongoji
kijulikanacho kwa jina la Moshono. Wito wa kupanda miti katika mlima huu
umeitikiwa kwa nguvu zote na miti hiyo hutunzwa kwa sheria ndogondogo
walizojiwekea wananchi wenyewe.
HOSPITAL YA TEMEKE NA WATU WALIOGANDANA
Watu waliokuwepo hospital ya Temeke wakitaka kuwaona watu waliogandiana
baada ya kusadikiwa walivunja amri ya sita.
ilikuwa kila baada ya dakika moja watu wanaongezeka
Hali ilivyokuwa katika barabara ya Temeke Hospital ikalazimika polisi
kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waliokuwepo hapo
Watu wakiwa katika barabara wakitaka kujua kinachoendelea
Ukuta umezingirwa
Barabara imefungwa mpaka naondoka eneo la tukio ukweli hasa haujajulikana
sababu kila unayemuuliza anaeleza anvyojua yeye kuhusu hilo suala la
kugandiana kwa watu hao wawili
Mazishi ya Twaha Kivumbi-Temeke
Twaha Jokolo akinena jambo wakati wa msiba huo wa rafiki yake Twaha
Kivumbi aliokuwepo maeneo ya changombe Temeke
Kicheko, Jax na Nyerere wakiwa katika msiba huo
Simon Butte (Mjo) likuwepo kumsindikiza rafiki yake
Banyai (Dubwi ) aliesimama
Salvatory Edward mwenyeshati la drafti akiwa na David Beatus, Peter Nkwera
na shaffih Magongo
Maiti ikisaliwa
Baadhi ya ndugu, jamaa na rafiki waliohudhuria katika mazishi ya ndugu yao
Twaha Kivumbi
Kenny Mwaisabula akiwa na baadhi ya viongozi wa Bandari katika msiba huo
TRA yakusanya shilingi 754 bilioni

Mwezi Septemba mwaka huu Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) imevunja rekodi ya
kukusanya kodi hadi kufikia shilingi 754 bilioni. Wanaongoza kwa kulipa
kodi ni National Microfinance Bank (NMB) wakifuatiwa na Tanzania Breweries
Limited (TBL) na Tanzania Cigarette Company Limited (TCC)
Pichani mmoja wa wafanyakazi wa NMB Business Centre (Picha kwa hisani ya
DailyNews 8/11/2012)
Obama umeliletea heshima Bara la Afrika

Kwa kuchaguliwa tena kwa mara ya pili kuwa Rais wa Marekani, Barack Obama
ameliletea heshima Bara la Afrika. HONGERA!
Pichani Rais Barack Obama akiwa na familia yake kutoka kushoto mkewe
Michelle, Sasha na Malia (Bintize)- Picha kwa hisani ya gazeti la Daily
News
'Jiko' kutoka Chamazi
Jumapili ya tarehe 4/11/2012 Bw. Salehe Pembe (Shemeji) alinunua jiko jipya
kutoka Chamazi.
Lengo ni moja
Iwe ni ndoa ya Kikristu au ya Kiislamu lengo ni moja ni kufunga ndoa.
Tunatofautiana katika taratibu.
Africana wakutana Kitunda
Mwezi Oktoba 2012- Kikundi cha Africana kilikutana huko Kitunda Jijini Dar
nyumbani kwa Gloria. Kikao kilifanyika kwa mafanikio makubwa. Wanachama
wameazimia kukamilisha michango yao ya kila mwezi kabla ya mwisho wa mwezi
wa Novemba, kutoa fedha za T-shirt za Africana pamoja na kununua hisa za
mradi wa SH2
No comments:
Post a Comment