Mkuu
wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia)
akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
(kushoto) kabla ya uzinduzi wa Supermarket ya kwanza katika Jeshi la
Magereza nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa Supermarket ya kwanza ya Jeshi la Magereza nchini.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Military Shop, Afzal Meghji akimuonyesha bidhaa
mbalimbali zilizopo ndani ya duka hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na maafisa
magereza (hawapo pichani) kabla ya kufungua Supermarket kubwa ya kisasa
ambayo itawawezesha maafisa hao, askari na familia zao kupata huduma ya
kununua bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa
wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, anayefuata ni Mkuu wa Jeshi la Magereza
nchini, John Minja na kulia ni Mwekezaji Mkuu wa Kampuni ya Military
Shops ambaye ndiye aliyewekeza katika Supermarket hiyo, Sadrunin Virji.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmauel Nchimbi akipokea zawadi kutoka
kwa mke wa Mwekezaji Mkuu wa Supermakert hiyo, Gulshan Virji (kulia).
Mkuu
wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali, John Minja akipokea
zawadi kutoka kwa mke wa Mwekezaji Mkuu wa Supermakert hiyo, Gulshan
Virji (kulia).
Baadhi ya maafisa na askari Magereza wakinunua bidhaa mbalimbali katika Supermakert hiyo baada ya kuzinduliwa.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa tatu kutoka kushoto
waliokaa), Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (wa kwanza
aliyekaa kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa mbalimbali wa
magereza pamoja na wageni waalikwa.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment